Skip to main content

Uwajibikaji kwa Jamii (CSR)

Uwajibikaji kwa Jamii (CSR)

Kuleta Athari Chanya Zaidi ya Takwimu

Airtel Tanzania imejizatiti kuleta mabadiliko chanya yanayozidi faida za kibiashara. Dhamira hii inatekelezwa kupitia mkakati maalum wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) chini ya Airtel Africa Foundation kupitia mfumo wa FEED.

Mfumo huu umejikita katika maeneo manne muhimu

Maeneo haya yanaonyesha dhamira ya Airtel Tanzania kuondoa vikwazo vinavyozuia jamii kunufaika na fursa zilizopo katika dunia ya kidijitali.

Kupitia nguzo hizi, Airtel Tanzania inawawezesha watu binafsi na jamii kwa kuwapatia zana, ujuzi na huduma muhimu ili waweze kufanikiwa. Kwetu sisi,Airtel Tanzania  mafanikio hayapimwi kwa takwimu tu bali kwa fursa, uimara na mabadiliko chanya.

 

Mradi wa Elimu wa Airtel SmartWASOMI

Kukuza upatikanaji wa elimu bora kwa njia ya kidijitali kwa shule za Sekondari

Mradi wa Airtel SmartWASOMI ni mpango wa elimu ya kidijitali unaofadhiliwa na Airtel Africa Foundation, unaolenga kubadilisha mfumo wa ujifunzaji nchini Tanzania kwa kuunganisha shule za sekondari za umma na intaneti yenye kasi kubwa pamoja na majukwaa ya kujifunzia mtandaoni.

Mradi Airtel SmartWASOMI unatekelezwa na Airtel Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF na Serikali ya Tanzania. Mpango huu wa miaka mitano unalenga kufikia shule 3,000, ambapo shule 1,000 zinatarajiwa kuunganishwa ifikapo mwaka 2025/2026. Hadi sasa, shule 534 tayari zimeunganishwa na mtandao Madhubuti wa Airtel.

Mradi Airtel SmartWASOMI umewanufaisha walimu 9,700 na wanafunzi 381,162 kupitia upatikanaji wa bure wa majukwaa manne ya elimu yasiyotozwa gharama za data. Aidha, kuna madarasa 50 ya kisasa (Smart Classes) yanayoendelea kuanzishwa.

Mradi wa Airtel SmartWASOMI unaunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu kwa kuingiza miundombinu ya kidijitali shuleni, kupunguza pengo la kidijitali, na kuendeleza mfumo jumuishi wa elimu unaotumia TEHAMA.

 

Elimu inayoendeshwa na AI kwa mustakabali wa kidijitali wa Afrika

Programu ya Airtel Africa Fellowship

Airtel Africa Fellowship ni mpango wa elimu wa kikanda unaoendeshwa na Airtel Africa Foundation kwa kushirikiana na IIT Madras – Tawi la Zanzibar, unaolenga kujenga uwezo wa Afrika katika sayansi ya data na akili bandia (Artificial Intelligence).

Ufadhili  wa  Airtel Africa Fellowship  unathamani ya dola za Marekani 500,000 unatoa scholarships kamili kwa wanafunzi 10 wa shahada ya kwanza kwa kipindi cha miaka minne, ukiweka mkazo mkubwa katika kuwawezesha wanawake na vijana wenye changamoto za kijamii.

Ukiwa Zanzibar, mpango wa unachangia kukuza nguvu kazi yenye ujuzi wa kidijitali kwa kupanua upatikanaji wa elimu ya juu ya STEM. Pia unaunga mkono juhudi za bara la Afrika za kuimarisha uongozi wa teknolojia, kupunguza pengo la ujuzi wa kidijitali, na kuharakisha mabadiliko kuelekea uchumi unaotegemea maarifa na ubunifu.

Kutana na wanafunzi wa Airtel Africa Fellowship  (Airtel Fellows) wanaofadhiliwa na Airtel Africa Foundation (picha)

 

Kukuza ajira kwa vijana kupitia mafunzo ya ufundi stadi kidijitali

Programu ya Mafunzo ya Ufundi ya Airtel VSOMO

Airtel VSOMO ni jukwaa la kwanza la kiditali linalotoa mafunzo ya ufundi stadi kupitia simu ya mkononi nchini Tanzania na ni jukwaa rasmi la kitaifa la mafunzo ya ufundi mtandaoni chini ya VETA kwa kushirikiana na Airtel Tanzania.

Mpango  Airtel VSOMOunawawezesha Watanzania kujifunza ujuzi wa ufundi stadi chini ya VETA wakati wowote na mahali popote kwa kutumia vifaa vya kidijitali kama vile simu, kompyuta mpakato, tablet na runinga janja (smart TV), kwa urahisi na kwa njia inayofikika kwa wengi.

Airtel VSOMO imeunganishwa na mifumo mingine muhimu ya VETA kama vile Fundi Connect, ambalo linaunganisha wahitimu moja kwa moja na fursa za ajira, hivyo kurahisisha mpito kutoka mafunzo hadi ajira.

Mpango huu, unaofadhiliwa na Airtel Africa Foundation kama sehemu ya CSR, unatoa mafunzo ya ufundi kidijitali bila gharama za data, na hadi sasa umewezesha zaidi ya wanafunzi 6,700 kupata maudhui ya kujifunzia bila malipo ya intaneti.

Katika kusaidia kukamilisha mkakati ya VETA katika kukuza ujuzi, VSOMO imejipanga  kufundisha wanafunzi 1200 kila mwaka ili kuimarisha na kupanua upatikanaji wa elimu ya ufundi stadi. Mpango huu unaongeza nafasi za ajira kwa vijana kwa kuunganisha mafunzo ya kidijitali na fursa halisi za ajira.

 

Kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa shule za msingi

Programu ya Airtel ShuleYetu ya Kuasili Shule(Airtel Adopt A School)

Huu ni mpango wa kusaidia elimu unaolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zenye uhitaji kupitia ukarabati wa madarasa na miundombinu ya usafi.

Airtel ShuleYetu kwa sasa ni mpango unatekelezwa katika maeneo kama Bagamoyo na Songwe,  ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza udahili na mahudhurio ya wanafunzi, pamoja na kuboresha matokeo ya elimu.

Katika Shule ya Kiromo baada ya ukarabati wa shule, idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka takriban 700 hadi zaidi ya 1,400, ikionyesha maboresho makubwa katika upatikanaji wa elimu na mazingira ya kujifunzia. Mkoa wa Songwe ukarabati unaendelea katika shule ya Msingi Mnyuzi unatarajiwa kuona ongezeko la wanafunzi kutoka karibu 400 hadi mara mbili baada ya ukarabati kukamilika.

Airtel Shule Yetu pia inatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa ufaulu wa kitaaluma, ikiwa ni pamoja na kuongeza viwango vya ufaulu wa mitihani kutokana na mazingira bora ya kujifunzia.

 

Kuwawezesha vijana na wanawake kupitia ujumuishaji wa kidijitali katika huduma za fedha

Airtel FursaLab – Elimu ya Fedha kwa Wanawake na Ujumuishaji wa Kidijitali kwa Vijana

Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) kwa kushirikiana na Airtel Money Tanzania inaendesha programu ya Airtel FURSALAB.

Airtel Fursa (Airtel FursaLab) ni mpango mkuu wa CSR wa Airtel Money Tanzania unaolenga kuiwezesha jamii kupitia upatikanaji wa fursa, kujengewa uwezo, na ujumuishaji wa kifedha.

Kupitia mpango wa Airtel FursaLab, Airtel Money Tanzania kwa ufadhili wa Airtel Africa Foundation inaunga mkono programu zinazoinua makundi yaliyopo pembezoni na kuchangia maendeleo ya taifa.

Lengo la Airtel FursaLab ni kuimarisha uwezeshaji wa kiuchumi na kijamii, hasa kwa wanawake na vijana, kupitia programu maalum zinazoongeza ujuzi, maarifa, na uendelevu wa muda mrefu.

Hadi sasa, zaidi ya washiriki 5,300 wamepata mafunzo ya elimu ya fedha na ujumuishaji wa kifedha. Airtel FursaLab inatekelezwa kupitia vituo vine kimoja Dar es Salaam na vitatu Zanzibar na hivyo kuongeza fursa kwa wajasiriamali katika maeneo muhimu.

 

Matumizi ya nishati safi na usimamizi bora wa taka

Utunzaji wa Mazingira kupitia Usimamizi wa Taka za Kielektroniki (E-Waste)

Airtel Tanzania inaendeleza utunzaji wa mazingira kupitia mradi wake wa E-Waste Go Green, ujulikanao kama Airtel Go-Green unaohamasisha usimamizi sahihi wa taka za kielektroniki kwa kutoa elimu ya uelewa na kuhakikisha utupaji salama wa taka, ukiungwa mkono na kampeni za ndani za urejelezaji.

Airtel Go-Green inalenga shughuli za Airtel nchini kote na kuhamasisha usimamizi bora wa taka za kielektroniki ili kupunguza madhara kwa mazingira.

Sambamba na hilo, Airtel imebadilisha zaidi ya asilimia 50 ya vituo vyake kutoka matumizi ya jenereta za dizeli kwenda kwenye umeme wa gridi ya taifa, hatua ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa chafu na kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati.

Airtel pia inashirikiana kwa karibu na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wateja wake kupitia ujumbe mfupi (SMS) kila mwaka.

Vilevile, mwaka huu Airtel kwa kushirikiana na NEMC wameanzisha programu ya “Let’s Go Green Together.” Kupitia mpango wa Airtel Go-Green , Airtel na NEMC wanatekeleza shughuli mbalimbali za kulinda na kutunza mazingira, ikiwemo kufanya usafi katika fukwe za bahari pamoja na kupanda miti ya matunda na miti ya kivuli katika shule na mikoa mbalimbali.

Katika mwaka huu, Airtel Go-Green programu  ilizinduliwa katika Shule ya Msingi Kiromo, Bagamoyo, ambapo miti 100 ilipandwa kama sehemu ya juhudi za kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Kwa pamoja, juhudi hizi zinaunga mkono uendeshaji endelevu kupitia matumizi ya nishati safi na usimamizi wa taka unaowajibika.