Kuzuru kwa malipo ya baadae | TZ
- Home
- Binafsi
- Malipo ya Baadaye (Postpaid)
- Kuzurui
Simu nyingi zinaweza kufanya kazi karibu kila sehemu duniani, lakini kuna baadhi ya nchi ambazo Airtel Tanzania haina makubaliano ya kimataifa ya roaming. Tafadhali rejea orodha ya nchi zenye huduma ya international roaming. Nenda kwenye (partner list).
Ndiyo, utahitaji kuchagua mtandao unaoutaka. Unaweza kuangalia waendeshaji wa mitandao (partner list) hapa.
Kwa wateja wa Postpaid: Utahitaji kuiwasha huduma hii katika ofisi ya Airtel Tanzania au kupiga simu kwa +255 78 4105401 ili kuwashwa (Inawezekana ukahitajika kuweka amana ya usalama kwa ajili ya roaming).
Kwa wateja wa Prepaid: Huduma ya International Roaming tayari huwa imewezeshwa kwenye laini yako. Hakikisha tu una muda wa kutosha wa maongezi kabla ya kuondoka nchini.
Mteja wa Prepaid anaweza kujaza salio akiwa roaming kupitia Airtel Money bila malipo yoyote.
Kupata muda wa maongezi, chagua “Buy airtime” kutoka kwenye menyu ya Airtel Money kwa kupiga *150*60# Familia na marafiki waliopo Airtel wanaweza pia kukujazia muda wa maongezi kupitia ME2U.
Unaweza kupiga simu popote ndani ya nchi unayotembelea kwa kupiga namba ya eneo (area code) kisha namba unayotaka.
Kupiga simu Tanzania: Piga +255 ikifuatiwa na namba husika. Mfano kwa Airtel mobile: +255 78x xxxxxx Kwa laini ya mezani (landline): +255 22 2xxxxxxx
Kupiga nchi nyingine: Piga + ikifuatiwa na country code + area code + namba Mfano: Kwa Uingereza piga +44 77xxxxxxxx
Kutuma SMS: Andika ujumbe wako na utume kwa namba kwa kutumia muundo kama ilivyo hapo juu.
ONE AIRTEL Roaming, inayopatikana kwenye nchi zilizo kwenye AIRTEL FOOTPRINT, hukuwezesha kutumia viwango vilivyopunguzwa unapokuwa nje ya nchi ambako Airtel ipo.
Unaweza kutumia laini yako ya Airtel katika nchi 17 zifuatazo: Kenya, Chad, Congo, DR Congo, Uganda, Rwanda, Madagascar, Shelisheli, Nigeria, Niger, Malawi, Zambia, Ghana, Gabon, Bangladesh, India na Sri Lanka.
Ndiyo, unaweza. Ukiwa na smartphone, zima tu Mobile Data halafu utaendelea kupiga na kupokea simu pamoja na SMS. Mfano wa kufunga data roaming:
iPhone: settings > network > data roaming > off
Samsung: menu > settings > network > mobile network > mobile data > off
Unapowasha simu kwa mara ya kwanza ukiwa nchi nyingine, unaweza kuona mitandao mingi. Lakini Airtel Tanzania haina makubaliano na mitandao yote. Utaweza kuunganisha tu kwenye mtandao ambao ni partner wetu kwenye nchi hiyo. Ukiwa umeweka Automatic Network Selection, simu yako itachagua mtandao wa partner wetu moja kwa moja.
Ikiwa simu yako haijiunganishi moja kwa moja, fuata hatua hizi:
Hakikisha kwenye settings umeweka Automatic Network Selection
Hakikisha upo maeneo yenye mtandao mzuri
Ipe simu muda hadi dakika 3 kujisajili kwenye mtandao
Simu yako sasa itajiunganisha kiotomatiki
Hii ni huduma inayowawezesha wateja kuendelea kuwasiliana wakiwa angani kwenye ndege, kwa kushirikiana na Aero-Mobile.
Wateja wa Postpaid waliowezeshwa roaming wanaweza:
- Kupiga na kupokea simu
- Kutuma na kupokea SMS
- Kutumia intaneti wakiwa kwenye ndege kwenye safari za kimataifa.
Gharama hutegemea nchi unayosafiri na mtandao utakaochagua kutumia. Hivyo, hakikisha umefahamu orodha ya mitandao washirika (partner list) na viwango vyetu vya bei kabla ya kusafiri.
Kwa wateja wa postpaid, gharama za roaming zitaongezwa kwenye bili yako mara tu tunapopokea taarifa za matumizi yako.
Kwa kuwa tunategemea mitandao ya nje kututumia taarifa za matumizi (data, simu na SMS), wakati mwingine kunaweza kuwa na ucheleweshaji kabla ya makato kuonekana kwenye akaunti yako.
Wakati mwingine hutoweza kuona makato haya kwenye bili inayofuata moja kwa moja.
Ndiyo, utatozwa kwa kupokea simu ukiwa kwenye mtandao wa nchi unayotembelea.
Ndiyo, kupokea SMS nikiwa roaming ni bure.
Unaweza kutupigia simu kupitia +255 78 4105401 (kwa Kiingereza) au +255 78 4105400 (kwa Kiswahili) kutoka simu yako katika nchi nyingi.
Ikiwa haitafanya kazi, unaweza pia kututumia barua pepe kupitia helpdesk@airtel.co.tz
Tafadhali tupigie simu kupitia +255 78 4105401 kutoka simu yoyote duniani ili kuweka vizuizi (bar) kwenye laini yako na kuzuia matumizi yasiyoruhusiwa.
Ukisharudi Tanzania, simu yako itafanya kazi kama kawaida ilivyokuwa kabla ya kusafiri.
Kumbuka…
Hakikisha umebeba kifaa cha kuchajia (power adapter) kinacholingana na nchi unayoitembelea ili uweze kuchaji simu yako.
Ni vyema kuhifadhi namba zako kwa kutumia msimbo wa kimataifa (Tanzania ni +255), ili uweze kuzipiga kwa urahisi ukiwa sehemu yoyote duniani.
Mfano: namba ya Tanzania 0784 XXX XXX inapaswa kuhifadhiwa kama +255 784 XXX XXX
Pia hakikisha kuwa umelipa bili zako zote kabla ya kuondoka nchini. Hii itahakikisha kuwa huduma yako ya simu haitaathiriwa ukiwa safarini.