eSIM | TZ
- Home
- Binafsi
- Usaidizi
- eSIM
- e-SIM ni mageuzi ya SIM ya kawaida yenye uwezo sawa; tofauti pekee ni kwamba ni ya kidijitali — hivyo kuondoa uwezekano wa kupoteza au kuharibu SIM.
- Inaweza kuwa SIM ya pili kwenye simu ambazo zina slot moja tu ya SIM ya kawaida.
- Ukiwa na kifaa kinachokubaliana na eSIM unaweza kuweka profaili ya eSIM kwa urahisi.
- Ikiwa wewe ni msafiri wa mara kwa mara, utagundua kuwa eSIM ni rahisi sana kwa kubadilisha mitandao ya simu.
- Mtu yeyote mwenye simu inayokubaliana na e-SIM.
- Mteja wa Airtel anaweza kubadilisha SIM yake ya kawaida kuwa e-SIM au kuchukua e-SIM ya ziada kwenye simu yake (kama laini ya pili).
- Mteja yeyote mwenye SIM ya kawaida kutoka mtandao mwingine pia anaweza kuchukua e-SIM ya Airtel endapo simu yake inakubaliana na e-SIM.
- Apple Watch / iPad / na vifaa vingine vinavyokubaliana na e-SIM.
- Kwanza, hakikisha kama simu yako inakubaliana na eSIM kwa kupiga *#06# kwenye simu yako.
- Kifaa chako kinapaswa kuonyesha namba ya EID – hii inaonyesha kuwa simu yako inaweza kutumia eSIM.
afanuzi
Utumizi
Upatikanaji
Tafadhali tembelea duka lolote la Airtel kufanya SIM Swap kutoka laini yako ya kawaida (physical SIM) kwenda eSIM.
Mteja anatakiwa kufika na Kitambulisho cha Taifa (NIDA ID).
Hapana, si vifaa vyote vinavyokubaliana na eSIM. Ni baadhi tu ya simu zilizochaguliwa zinazokubalika.
Piga #06#. Ikiwa kifaa chako kitaonyesha namba ya EID, basi simu yako inaweza kutumia eSIM.
Ndiyo, ukiwa na laini zote mbili hai, inamaanisha una namba mbili tofauti kwenye simu moja. Hii inafanya kifaa chako kuwa Dual SIM.
Ndiyo, unaweza kupiga na kupokea simu na ujumbe kutoka kwenye namba zote mbili. Hata hivyo, ukiwa kwenye simu kwa kutumia namba moja, simu inayoingia kwenye namba ya pili itaenda voicemail, na pia utapata taarifa ya simu uliyoikosa. Call Waiting itafanya kazi endapo simu inayoingia ni ya namba ileile unayotumia kwa wakati huo.
Ndiyo, shughuli zote hizi na nyingine nyingi zinaweza kufanyika kwenye eSIM mara tu inapowashwa.
Hapana, unahitaji kutembelea duka la Airtel ili kununua eSIM na kufanya SIM Swap.
Hapana, lazima uwe umeunganishwa na Wi-Fi au mtandao wa simu ili kupakua QR code.
Ndiyo, matumizi ni sawa na laini ya kawaida ambapo unaweza kubadilisha kati ya mitandao hiyo.
Hii inategemea kifaa husika kutokana na utofauti wa vipengele na uwezo wa watengenezaji.
Hapana, utatakiwa kutumia menyu ya My Airtel App ili kuhuisha akaunti yako ya Airtel Money baada ya SIM Swap.